Majeraha kumuweka nje Mo Salah hadi kombe la dunia
Eric Buyanza
April 28, 2026
Share :

Mkurugenzi wa timu ya Taifa ya Misri, Ibrahim Hassan amesema Mohamed Salah anaweza kukaa nje ya uwanja hadi litakapoanza kombi la Dunia, baada ya kuumia nyama za paja kwenye mchezo dhidi ya Cystal Palace Jumamosi iliyopita.
Liverpool bado hawajatoa taarifa rasmi juu ya nyota huyo ambaye anaondoka msimu huu wa joto baada ya miaka tisa huko Anfield.
Kwasasa timu hiyo inashika nafasi ya nne kwenye Ligi kuu wakiwa na pointi 58 na wanatazamiwa kufuzu Ligi ya Mabingwa, huku wakiwa na pointi nane mbele ya Brighton walio nafasi ya sita.
Watamenyana na Manchester United na Aston Villa wakiwa ugenini na watawakaribisha Chelsea na Brentford katika uwanja wa Anfield - ambao ungekuwa mchezo wa mwisho kwa Salah.





