pmbet

Majeraha yafanya mechi ya Stars na Morocco kuahirishwa

Sisti Herman

October 4, 2026
Share :

 

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kufutwa kwa mechi ya kimataifa ya kirafiki baina ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Morocco.

Mechi hiyo ilipangwa ichezwe Jumatatu, Oktoba 5, 2026 jijini Tangier, Morocco.

Hata hivyo TFF imesema kwamba mchezo huo hautokuwepo kutokana na Taifa Stars kutokuwa na idadi ya kutosha ya wachezaji.

“Uamuzi wa kufuta mchezo huo umetokana na ripoti ya madaktari wa Taifa Stars wakati wakielezea hali ya wachezaji waliopo kambini kwenye mji wa Tangier.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wachezaji watano wamepata majeraha ambayo yatawafanya washindwe kucheza mchezo huo dhidi ya Morocco.

“Baada ya kushauriana na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi tumekubaliana kuufuta mchezo huo," imesema TFF

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet