Majeruhi yamuumiza akili Ten Hag United
Sisti Herman
April 21, 2024
Share :
Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema kuwa kwa kipindi cha miezi 18 kilichopita kile anachoamini kuwa ni kikosi chake bora hakijawahi kucheza pamoja kwasababu ya ingia toka za wachezaji kwasababu ya majeraha ya mara kwa mara.
"Kwenye miezi 18 iliyopita sijawahi na wachezaji nnaowahitaji kwenye kikosi changu cha kwanza wote kwa pamoja uwanjani kwasababu ya kusumbuliwa na majeraha, leo huyu, kesho yule" alisema Ten Hag.
Kocha huyo wa Man Utd ameyasema hayo jana wakati wa mkutano na wanahabari wakijiandaa na mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Coventry ambapo watawakosa nyota kadhaa wa kikosi cha kwanza kama Raphael Varane, Lisandro Martinez, Luke Shaw, Victor Lindalof na wengineo.
United ikishinda watakutana na City kwenye Fainali ya michuano hiyo itakayochezwa wembley.