Majibizano ya Bellingham na Romero yawaibua mashabiki wa Messi.
Joyce Shedrack
September 22, 2026
Share :
Mshambuliaji wa Real Madrid Jude Bellingham na mchezaji wa Atletico Madrid Cristian ‘Cuti’ Romero walionekana kutupiana maneno makali katika tukio lililozua mvutano mkubwa, huku mazungumzo yao yakidaiwa kufichuliwa na Movistar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Bellingham alimchokoza Romero wakati wa mchezo wa Madrid Derby huku baadhi ya mashabiki wakihoji imekuaje Bellingham akamuingiza Messi kwenye mzozo huo.
Majibizano hayo yalikuwa hivi“ Wewe ni mtoto wa kulia! Nenda kalie tena!”
Romero hakubaki kimya, akimjibu kwa kumkumbusha Bellingham kuhusu tukio la Kombe la Dunia, akisema:
“Lia, lia… tayari ulilia kule Kombe la Dunia.”
Bellingham akaendelea kumchokoza beki huyo wa Argentina kwa kumtaja Lionel Messi, akisema:
“Messi akiwa karibu nawe unaongea sana, eh… hapa, sifuri!”
Romero naye akafunga mjadala huo kwa kumwambia Bellingham“Lia, lia, lia… kaa kimya. Nyamaza.”
Unadhani Bellingham alikuwa sahihi kumtaja Lionel Messi Nahodha wa Argentina kwenye mzozo huo?.





