Majizzo ajilipua kuwaombea msamaha wasanii.
Joyce Shedrack
December 11, 2025
Share :
Mdau wa muziki Nchini na mmiliki wa TVE na EFM Majizzo amefanya mkutano na waandishi wa habari akiwaombea radhi wasanii wa muziki Nchini kwa maneno yaliyowakera wananchi hadi kupelekea kazi zao kutokufanya vizuri tena kwenye majukwaa ya muziki.

Majizoo ameweka wazi kuwa anaelewa kuna maneno yaliyowakera wananchi ambao ndio mashabiki halisi wa muziki hivyo anawaomba Watanzania wawasamehe na waendelee kuwaunga mkono kwenye kazi zao.
“Msamaha ninaoomba ni kwa sababu nafahamu kuna mahali wadogo zangu hawa walipitiliza na sio kwa sababu walifanya kampeni (ile ni haki yao na uamuzi wao). Najua kuna maneno yalikukera, sio katika level ya siasa, bali katika level ya utu. NAOMBA MSAMAHA”.
“Huu muziki ni wenu. Mkiumiza tasnia, mnaumiza maelfu ya ajira. Kina Shilole hao wanaweza kutufikia sisi siku moja moja ukamtoa, vipi kuhusu wale wafanyakazi wake? Diamond na wengine, Mungu amewajaalia riziki, lakini unawaza kuhusu ajira zinazopotea kwa sababu ya hasira yako kwake?”.
“Naomba Radhi, na ikiwapendeza naomba muendelee kuupa nguvu Muziki wenu”.





