pmbet

Makahaba waiambia serikali wako tayari kulipa kodi

Eric Buyanza

May 24, 2024
Share :

Makahaba nchini Kenya wanaofanyia shughuli zao katika mji wa Thika, wameiambia serikali ya Kenya inayoongozwa na Rais William Ruto kuwa wako tayari kulipa kodi ya serikali kutokana na biashara yao.

Makahaba hao pia wakajiongeza na kupendekeza kodi watakayotozwa iwe kati ya Sh200 na Sh400 kwa siku, (400 ya Kenya ni sawa na Sh 7,800 za Tanzania).

Mwakilishi wa makahaba hao, Bi Anne Wambui, amesema ushuru huo walioupendekeza ni sawa na pesa ambazo wanatozwa na baadhi ya polisi kila siku.

Bi Wambui alisema biashara hiyo imewakusanya pamoja wanawake wapatao 1,000 ambao kila siku wanaweza kuipatia serikali ushuru wa kati ya Sh73 milioni na Sh146 milioni.

Alisema badala ya vita vya kila siku kati ya serikali na wanawake hao wanaojiuza, ifike mahali sasa waelewane jinsi watakavyoshirikiana ili wao wapate riziki na serikali nayo ipate kodi.
TAIFALEO

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet