Makalla afunguka Rais Mwinyi kuongezewa muda madarakani Zanzibar
Sisti Herman
June 24, 2024
Share :
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ametoa tamko kwa niaba ya chama hicho kuhusu habari zinazosambaa kwa kasi kwenye vyombo va habari na mitandao ya kijamii kuhusu Rais wa Zanzibar kutaka kuongezewa muda wa kukaa madarakani.
"Taarifa zinazosambaa hazipo katika utaratibu wa vikao vya chama chetu na niliovyosoma nimeelewa kwamba ni mawazo hata kile kikao cha Zanzibar ambacho ni kamati maalum ambayo mwenyekiti wake anakuwa Makamu mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar nako halijafika" alisema Makalla.
Makalla ametoa ufafanuzi huo leo, Juni 24, 2024 akiwa kwenye mahojiano maalum na Mtangazaji Richard Ngailawa Global Tv kwenye kipindi cha Global Exclusive aliyetaka kujua msimamo wa chama hicho kuhusu suala hilo.