pmbet

Makamu wa Rais awasili msibani kwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro.

Joyce Shedrack

June 19, 2024
Share :

Makamu wa Rais wa Tanzania Dk Philip Mpango amewasili nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Tixon Nzunda (56) aliyefariki dunia kwa ajali siku ya jana katika eneo la Njia Panda ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akienda kumpokea Makamu wa Rais Dk Philip Mpango ambaye alikuwa akielekea mkoani Arusha kikazi.
 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa siku ya jana alithibitisha kutokea kwa ajili hiyo akitaja  chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa lori aina ya Scania mali ya Oronge Gas kushindwa kulimudu gari lake na kwenda kugonga gari la RAS na kusababisha ajali hiyo.

 

Katibu tawala huyo alifariki dunia pamoja na dereva wake  Alphonce Edson mwenye umri wa miaka 54.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet