pmbet

Makamu wa Rais wa Marekani atangaza kupata mtoto wa 4

Eric Buyanza

July 20, 2026
Share :

Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance, ametangaza kuzaliwa kwa mtoto wake wa nne, mvulana aliyepewa jina la Alec Neel Vance.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X siku ya Jumapili, Vance alisema mke wake, Usha Vance, pamoja na mtoto huyo wako katika hali nzuri baada ya kujifungua.

 

Pia alitoa shukrani kwa timu za madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Kijeshi ya Walter Reed National Military Medical Center pamoja na Kitengo cha Afya cha Ikulu ya White House kwa huduma walizotoa wakati wa kujifungua.

 

"Tunafuraha kutangaza kuwa mtoto wetu wa kiume, Alec Neel Vance, amezaliwa asubuhi ya leo. Usha na mtoto wako salama na wenye afya njema, na watoto wetu wengine wana furaha kubwa kumpokea mdogo wao," aliandika Vance.

 

JD Vance na mkewe Usha tayari wana watoto wengine watatu ambao ni Ewan, Vivek na Mirabel, hivyo kuzaliwa kwa Alec kunafanya familia yao sasa kuwa na watoto wanne.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet