Makombora ya Urusi kuelekea Kharkiv, yasambaratisha hoteli
Eric Buyanza
January 11, 2024
Share :
Makombora Urusi yameshambulia hoteli katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, Kharkiv, na kujeruhi watu 11.
Kwa mujibu wa Gavana wa Kharkiv, Oleh Synehubov waliojeruhiwa ni pamoja na waandishi wa habari wa Uturuki.
Katika siku za hivi karibuni Urusi imeongeza mashambulizi ya anga kwa Ukraine, huku maafisa wa Ukraine wakisema makumi ya raia wamekufa katika mashambulizi hayo.
Mji Kharkiv upo kilomita 30 kutoka mpaka wa Urusi.