pmbet

Makonda akutana na Rais wa Barcelona.

Joyce Shedrack

September 15, 2026
Share :

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, ameanza ziara maalum ya siku nne katika Klabu ya FC Barcelona nchini Hispania kwa mwaliko wa Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta.

Makonda ameanza ziara hiyo tarehe 14 Septemba 2026 kwa kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu kuhusu fursa za ushirikiano katika maendeleo ya soka nchini Tanzania na kukabidhiwa jezi ya timu hiyo yenye jina la Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Mazungumzo ya Waziri Makonda na Laporta yalijikita katika maeneo ya kukuza vipaji, maendeleo ya kiufundi, uendeshaji wa timu ya taifa, pamoja na namna uzoefu wa Barcelona unavyoweza kusaidia maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Katika ziara hiyo, Rais Laporta pia amempatia Makonda salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Mzee Hafidh Ameir Hassan, kilichotokea tarehe 7 Septemba 2026.

Makonda amekwenda safari hiyo akiwa ameambatana na Wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na anatarajiwa kushuhudia mchezo kati ya Barcelona na Racing Santander utakaochezwa tarehe 16 Septemba 2026 katika Uwanja wa Camp Nou, jijini Barcelona, akiwa na mwenyeji wake Laporta.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet