pmbet

Makonda akutana na wachezaji wa Barca

Sisti Herman

September 20, 2026
Share :

 

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda amehitimisha ziara yake ndani ya Klabu ya Barcelona kwa kukutana na wachezaji wa kikosi cha kwanza wa timu hiyo.

Makonda alienda nchini Hispania kwa mualiko maalum wa Rais wa Barcelona, Juan Laporta na kufanya nae vikao mbalimbali vya maendeleo ya mpira wa Tanzania.

Katika wachezaji hao Makonda alionekana kuzungumza kwa ukaribu zaidi na staa wa timu hiyo na kikosi cha Washindi wa Kombe la Dunia 2026, Hispania, Lamine Yamal.

Akihitimisha ziara yake ya kihistoria, Makonda aliwaalika mmoja mmoja kuja kutembelea Tanzania na kujionea uzuri, utamaduni na vivutio vya kipekee vya nchi yetu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet