pmbet

Makonda ataja mpango wa El Clasico kuchezwa Arusha au Zanzibar

Sisti Herman

November 17, 2026
Share :

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amefichua mpango kabambe wa kuzileta klabu vigogo za soka nchini Uhispania, FC Barcelona na Real Madrid, kuja kucheza mechi za kirafiki nchini Tanzania katika mfumo wa nyumbani na ugenini.

​Akizungumza kuhusu mpango huo, Waziri Makonda amebainisha kuwa wazo hilo linachagizwa na ushabiki wao binafsi wa timu hizo, ambapo yeye ni shabiki wa FC Barcelona huku Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, akiwa shabiki wa Real Madrid.

​"Mimi ni shabiki wa Barcelona na pia Rais Mwinyi anaishabikia Madrid. Kwa hiyo nataka nizungumze naye kesho ili kuona uwezekano wa kucheza mechi ya Madrid na Barcelona," amesema Waziri Makonda.

​Kwa mujibu wa maelezo ya Waziri Makonda, katika mpango huo wa kihistoria, Real Madrid watakuwa wenyeji visiwani Zanzibar huku FC Barcelona wakiwa wenyeji jijini Arusha.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet