Makonda awasili Paris kwenye tamasha la utamaduni wa mswahili
Eric Buyanza
July 6, 2026
Share :
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amewasili katika viunga vya Eiffel Tower jijini Paris, Ufaransa, kwa ajili ya Tamasha la Utamaduni wa Mswahili linalofanyika leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani, Julai 7, 2026.
Tamasha hilo limejumuisha maonesho ya vyakula vya Kiswahili, kazi za sanaa, burudani za wasanii mbalimbali na shughuli zinazoonesha utajiri wa utamaduni wa Kiswahili. Mhe. Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kulihutubia tamasha hilo mbele ya wageni kutoka Tanzania na Ufaransa.





