Makonda kumkodishia Prof Jay nyumba maeneo ya Upanga
Eric Buyanza
December 23, 2023
Share :
Katibu wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amemuahidi aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi na msanii wa muziki HipHop, Joseph Haule (Prof Jay) kumtafutia nyumba karibu na Hospitali ya Muhimbili.
Makonda alitoa ahadi hiyo jana alipokwenda kumtembelea Prof Jay nyumbani kwake Mbezi Jijini Dar es salaam, baada ya msanii huyo kuelezea changamoto anazozipata za umbali kutoka Mbezi hadi kufika Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu.
Makonda amemuahidi Prof Jay kumtafutia nyumba na kumlipia maeneo ya Upanga ili kusudi aweze kuepukana na changamoto hiyo anayoipitia.
Pia mwenezi Makonda ametimiza ahadi yake ya kumchangia Sh milioni 10 Professor Jay, na kutoa kiasi kingine cha fedha cha Shilingi milioni 10 ikiwa ni mchango kutoka kwa ndugu wa Mwenezi huyo na hivyo kupelekea jumla ya mchango wote aliotoa kuwa milioni 20.