MAKONDA: Wapinzani wasipofanya mikutano nakosa maana!
Eric Buyanza
December 21, 2023
Share :
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda akiongea leo na wanahabari amesema yeye kama wapinzani wasipofanya mikutano ya hadhara thamani yake kwenye chama inapotea.
“Mimi hapa nilipo wapinzani wasipofanya mikutano ya hadhara umaana na thamani yangu kwenye chama inapotea, yaani mimi thamani yangu inaongezeka kunapokuwa na mikikimikiki, ndiyo maana watu wanasema oooh Makonda kaenda wapi, sasa jamani nashindana peke yangu? wenzangu siwaoni, niwaalike 2024 twendeni kazini jamani tunakula ruzuku za watu,”anamalizia.