Malalamiko ya umeme mwakani yatapungua - Rais Samia
Sisti Herman
December 17, 2023
Share :
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora usiku huu December 17,2023 Jijini Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba hadi kufikia miezi ya katikati mwakani 2024 malalamiko kuhusu umeme yatakuwa yamepungua kwakuwa vinu viwili vitawashwa katika Bwawa la Nyerere na kuongeza umeme kwenye gridi ya Taifa hivyo Nchi itakuwa na umeme wa kutosha.
“Itakapofika January mwakani tunaanza kuwasha kinu cha kwanza cha umeme pale kwenye Bwawa la Nyerere, jumla vinu vyote viko tisa, cha kwanza kitawaka January, cha pili hatutozidi April tutakuwa tumewasha kinu cha pili na vile viwili tukiwasha tutakuwa na umeme wa kutosha sana”
“Kwahiyo pamoja na jitihada nyingine za gesi, solar na mambo mengine lakini kwenye umeme wa maji ambao tunautegemea, nadhani katikati ya mwakani na ni malalamiko mengi (ya umeme) yatakuwa yamepungua, tutawasha vinu viwili tutaongeza kwenye gridi ya Taifa umeme mkubwa”