Malawi yampeleka Miss World binti wa Waziri badala ya mshindi wa Miss Malawi.
Joyce Shedrack
September 7, 2026
Share :
Nchi ya Malawi impeleka binti wa Waziri aitwaye Ireen Navicha kushiriki shindano la Miss World, badala ya Miss Malawi ambaye ni Thandi Chisi aliyeshinda taji la Miss Malawi mwezi Desemba 2025.

Waandaaji walidai sababu za kumpeleka Ireen Navicha mshindi wa pili na binti wa Waziri wa Jinsia, Mary Navicha kwenye Miss World ni kutokana na Thandi kuwa na umri mkubwa kupita kiasi (miaka 27) ingawa umri unaoruhusiwa kushiriki kwenye shindano hilo kubwa la ulimbwende duniani.
Washiriki wengine wenye umri wa miaka 27 walioshiriki ni pamoja na mwakilishi wa Afrika Kusini ambaye alifanikiwa kuingia katika kundi la washiriki sita bora. Baada mjadala kuibuka na kuwa gumzo kubwa mitandaoni wamedai kuwa Ireen alikuwa na uzoefu mkubwa zaidi katika mashindano ya urembo na wamekanusha kuhusika kwa siasa wala kuwepo kwa agizo la wazi kutoka kwa mama yake.
Watu na wadau mbalimbali wameonesha hasira zao mitandaoni wakihoji kuhusu uwazi na usawa wa mchakato uliotumika akiwemo Mbunge mmoja alijaribu kulizungumzia suala hilo bungeni lakini akazuiwa kuendelea. Navicha alifanikiwa kuingia hatua ya Top 40 na kuandika historia ya kuwa Mmalawi wa kwanza kufika hatua hiyo katioa historia ya Miss World.





