Malema; Tunataka Afrika iwe na Rais mmoja
Sisti Herman
September 2, 2025
Share :
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wanasheria wa Nigeria uliofanyika katika mji wa Enugu siku ya Jumapili, Julius Malema ambaye ni kiongozi wa chama upinzani cha EFF nchini Afrika Kusini, alielezea mipaka ya sasa ya Afrika kama “mipaka ya kikoloni” na kusema kuwa inapaswa kuvunjwa ili kuruhusu bara la Afrika kuzungumza kwa sauti moja.
Alisisitiza kuwa sarafu ya pamoja ya Afrika itakuwa imara zaidi dhidi ya sarafu za kimataifa, na kuongeza: “Hatujali Donald Trump au kiongozi mwingine yeyote anafikiria nini kutuhusu. Waafrika lazima wakatae kuwa vibaraka wa mataifa mengine. Lazima tusimame pamoja wakati dunia inabadilika na tuuonyeshe ulimwengu kuwa Afrika ni moja na ni sawa na mataifa mengine yote.”