"Malengo yangu ya leo ni kupata bao la ugenini" - Fadlu
Eric Buyanza
April 2, 2025
Share :
Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema wataingia kwenye mchezo wa leo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry, Uwanja wa Suez Canal kwa lengo la kupata bao la ugenini.
Fadlu alisema anaamini mchezo wa marudiano utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Aprili 9 ndio utakaoamua timu itakayoingia robo fainali, hivyo ni muhimu kwao kupata bao la ugenini kwenye mchezo wa leo.
“Naamini mchezo wa marudiano nyumbani utaamua timu itakayoingia robo fainali, hivyo malengo yangu kwenye mchezo wa leo ni kujaribu kupata bao la ugenini,” alisema Fadlu.
TSN