pmbet

Mali anazomiliki Victor Wanyama!

Eric Buyanza

December 5, 2023
Share :

Mwanasoka wa kulipwa Victor Mugubi Wanyama wa nchini Kenya, ni moja wa wachezaji Afrika mashariki anayeishi maisha ya kifahari kutokana na mali anazomiliki.


Baadhi tu ya mali anazomiliki ni pamoja na;


Volkswagen Crafter CR53 Maxi 
Gari lina skrini za televisheni za 3D, kitengeneza kahawa, friji, na kamera za CCTV za ndani na nje. Gari hilo libeba watu 10.


Mercedes Benz ML350 
Mashine ya kijerumani inakuja na V6 ya lita 3.5. Gari linaweza kuongeza kasi kutoka sifuri hadi 96km/saa kwa chini ya sekunde tisa. Kasi yake ya juu ni 225 km/saa.


Hummer H3 Hummer H3 
Ni gari lingine katika mkusanyiko wa Wanyama. Muundo wa H3 unagharimu kati ya KSh 17 milioni na KSh 32 milioni, kutegemea mwaka wa uzalishaji.


Range Rover Sport 
Hili ni gari lingine la kifahari ambalo mwanasoka huyo ameonekana akiliendesha mara nyingi. Gazeti la Daily Nation la nchini Kenya liliwahi kuripoti kuwa gari hilo liliwahi kuibiwa lakini baadaye lilipatikana.


Wanyama pia anamiliki magari aina ya Bentley na Cadillac Escalade, bila kusahau nyumba za kifahari anazomiliki Kenya na London Uingereza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet