"Malone bado yuko sana msimbazi haendi popote" - Wakala
Eric Buyanza
April 11, 2024
Share :
Baada ya tetesi kuwa beki wa kati wa Simba, Che Fondoh Malone, kuwa anataka kuondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, wakala wa mchezaji huyo, Amadou Fontem Tigana, amesema mchezaji huyo atasalia kwenye kikosi hicho kipindi chake chote cha mkataba, labda kama klabu yenyewe itataka kumuuza.
Akizungumza kutoka nchini Cameroon, kutokana na madai hayo, Amadou amesema baadhi ya wanahabari walimnukuu vibaya, badala yake alisema atacheza kwa juhudi kubwa ili klabu kubwa zimnunue.
"Hajasema kuwa haipendi Simba na wala hataki kuondoka Simba, bali watu wamemtafsiri vibaya, alichosema ni kwamba atacheza kwa juhudi kubwa ili klabu kubwa zimnunue," alifafanua wakala huyo.
Ufafanuzi huo unakuja siku moja tu baada ya baadhi ya vyombo vya habari kudai kuwa beki huyo ameandika barua ya kuomba kuondoka klabuni hapo mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu msimu huu.