Mama ahukumiwa jela kwa kumlazimisha binti yake kuolewa.
Joyce Shedrack
July 29, 2024
Share :
Mama mwenye umri wa miaka 40 Sakina Muhammad Jan raia wa Australia amekuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kukutwa na hatia ya kumshurutisha binti yake mwenye umri wa miaka 21 kuolewa na mwanaume ambaye baadae alimuua.
Mwanamama huyo alipatikana na hatia ya kumlazimisha Ruqia Haidari kuolewa na Mohammad Ali Halimi mwenye umri wa miaka 26 mwaka 2019 baada ya kubadilishana kiasi cha fedha na mwanaume huyo aliyemuoa binti yake.
Wiki sita baada ya harusi Halimi alimuua mke wake wake na alipatikana na hatia ambayo ilisababisha kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Siku ya Jumatatu Bi Sakina Jan ambaye alikana hatia alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kile hakimu alichokiita “Shinikizo lisilovumilika” aliloweka kwa binti yake.
Bi Sakina anakuwa mtu wa kwanza kufungwa jela chini ya sheria inayopinga ndoa ya lazima nchini Ausralia iliyopitishwa mwaka 2013 inayoambatana na adhabu ya kifungo cha miaka 7 jela kwa mtu atakayekutwa na hatia.