pmbet

Mama aliyemuua binti yake kisa kukataa kuolewa na binamu akamatwa

Eric Buyanza

June 1, 2024
Share :

Mwanamke mmoja aliyepatikana na hatia ya kumuua bintiye nchini Italia amekamatwa nchini Pakistan baada ya kujificha kwa miaka mitatu.

Disemba mwaka jana, Mahakama ya Italia ilimhukumu Nazia Shaheen kifungo cha maisha bila yeye kuwepo Mahakamani , kwa kosa la mauaji ya binitiye Saman Abbas.
 

Shaheen na mumewe, Shabbar Abbas, walimuua binti yao baada ya kukataa kuolewa na binamu yake kama walivyotaka wao.

Baada ya kufanya mauaji hayo wawili hao walitorokea nchini Pakistan, ambapo baadae Abbas alipatikana na kurudishwa nchini Italia Agosti 2023 huku mkewe  Shaheen akiueupuka mkono wa dola.
 

Lakini wiki hii, katika operesheni iliyohusisha Interpol na Polisi, mama huyo alinaswa kwenye kijiji kilicho karibu na mpaka wa Kashmir.

Alifikishwa mahakamani siku ya Ijumaa jijini Islamabad, huku taratibu za kumrejesha Italia zikiendelea.
 

Taarifa zinaeleza kuwa kabla ya kufanya mauaji hayo, wazazi wa binti huyo waligundua kuwa mtoto wao amepata mchumba tayari hapo Italia.

Kitendo hicho kiliwachukiza na kumuamuru  asafiri kwenda Pakistani ili akaolewe na binamu yake lakini binti huyo alikataa.
 

Waendesha mashtaka wanasema miezi kadhaa baadae baada kukataa kwenda kuolewa na binamu, binti huyo alitoweka asijulikane alipo.

Mwili wake ulikuja kupatikana Novemba 2021, jirani na nyumba ya wazazi wake walipokuwa wakiishi, baada ya mjomba wa marehemu kufichua alikozikwa.

Uchunguzi wa maiti yake uligundua alikuwa amevunjika mfupa wa shingo, labda kutokana na kunyongwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet