pmbet

Mama anaoga mbele ya binti yake, ili kumuonyesha mwili halisi unavyofanana

Eric Buyanza

April 20, 2024
Share :

Katika hali ya kushangaza Mwanasaikolojia aliyefahamika kwa jina la Angela Karanja, amekuwa na mazoea ya kuoga mbele ya binti yake wa miaka 18 anayeitwa Dee.

Angela mwenye umri wa miaka 48, amekuwa akivua nguo mbele ya Dee tangu akiwa mtoto na anasema anafanya hivyo ili kumuonyesha jinsi mwili halisi unavyofanana, kwani ile miili anayoiona kwenye mitandao ya kijamii si ya kweli.

"Miili yetu ni vyombo ambavyo tunapaswa kuishi ndani. Hiki ndicho tulicho nacho, tunapaswa kufurahi na kujivunia.

"Wazo langu ni kumuonyesha ukweli ulivyo na anapoona picha zilizohaririwa mtandaoni haziwezi kumtisha."

Binti huyo Dee Karanja anasema: “Hii imenifanya nijisikie vizuri kwa sababu sasa najua ukweli ulivyo...Tunaweza tusiipende miili yetu kila wakati lakini hata hivyo tunapaswa kuiheshimu kwa sababu tuna mwili mmoja tu"

"Ikiwa tunapenda miili yetu basi haijalishi mtu yeyote atasema nini hatutajisikia vibaya."

Angela anasema kuoga mbele ya binti yake tangu akiwa mdogo kumesaidia binti huyo kujiamini" na kuwa na furaha na mwili wake.

Alisema: “Tunapaswa kuwasaidia vijana wetu kujipenda jinsi walivyo”

Angela anasema huwa anatembea uchi akiwa nyumbani, na wala binti yake hashtuki na hii ni kutokana na malezi aliyompa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet