pmbet

Mama Lishe waahidi kumpa kura zote Mama Samia

Sisti Herman

September 15, 2025
Share :

 

Katibu wa Umoja wa Mama Lishe Wilaya ya Singida Mjini, Ndg. Dorcus, ameahidi kuwa mama lishe wote watajitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya kazi kubwa na yenye mafanikio makubwa katika awamu yake ya kwanza, hivyo mama lishe hawana shaka kumchagua tena kwa kishindo ili aendelee kuongoza taifa.

Kauli hiyo aliitoa katika kikao cha Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe Taifa, Ndg. Geofrey Kiliba, na Mama Lishe wa Wilaya ya Singida Mjini, ambapo walikubaliana kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani na kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa uchaguzi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet