Mama wa 2Face adai mwanae amerogwa atoa onyo kali.
Joyce Shedrack
March 12, 2025
Share :
Rose Idibia, Mama mzazi wa msanii nguli wa muziki kutoka Nigeria, Innocent Idibia, anayefahamika kwa jina la kisanii, 2Face, aomba Wanigeria wenzie kumsihi Natasha Osawuru, mjumbe wa Bunge la Jimbo la Edo kumwacha mwanawe.
Mama huyo, ambaye alidai kuwa huenda mwanawe hafanyi mambo yake katika akili zake zinazofaa, alimtaka mbunge huyo kuondoa shanga ulizoweka mkononi na shingoni kwa mwanae.
Akiingia kwenye mzozo huo, Bi Idibia alisema mwanawe kwa sasa hayuko sawa kimawazo kutokana na taratibu za talaka na mkewe waliyeachana naye.
"Habari za jioni, Wanaijeria. Jina langu ni Bibi Rose Idibia, mama wa 2face. Ujumbe huu ni wa Bi Natasha Osawaru wa Jimbo la Edo, ninatoa wito kwa akina mama wote nchini Nigeria wanisaidie kumsihi amwachie mwanangu.
“Mwanangu anapitia mchakato wa talaka, na ni wazi hayuko katika akili zake sawa sasa namfahamu mwanangu vizuri, Huyo si yeye.
"Tafadhali Natasha, shanga ulizoweka kwenye mkono wake na shingoni mwake, ziondoe na kumwachilia," alisema mama wa 2face.