Mama wa miaka 68 ajifungua mtoto wake wa kwanza
Eric Buyanza
March 13, 2024
Share :
Huko mjini Abeokuta nchini Nigeria, Mwanamke mwenye umri wa miaka 68 amefanikwa kujifungua mtoto wake wa kwanza.
Inaelezwa kuwa mama huyo amekuwa akitafuta mtoto kwa miaka mingi toka ujana wake lakini ilishindikana na kupelekea kukata tamaa akiamini ataondoka duniani bila kuitwa mama.
Hata hivyo wale wahenga waliosema 'Mungu si Athumani' hawakukosea, kwani mama huyo mungu alimpa uwezo wa kushika ujauzito na wiki iliyoisha akampa uwezo wa kujifungua salama.
Video iliyosambaa mtandaoni inamuonyesha mama huyo akizunguka kwenye chumba cha hospitali akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua, na video nyingine ikimuonesha akiwa amebeba kitoto kichanga.
Erramatti Mangamma wa Hyderabad nchini India, mpaka sasa bado anashikilia rekodi ya kuwa mama mwenye umri mkubwa zaidi aliyejifungua akiwa na umri wa miaka 73 kupitia njia ya upasuaji.