Mama wa Michael Jackson apata gawio la urithi
Sisti Herman
March 24, 2024
Share :
Baada ya mama mzazi wa marehemu mfalme wa Pop Michael Jackson (MJ), Katherine Jackson (93) kukata rufaa dhidi ya wasimamizi wa mali za MJ, hatimaye wasimamizi wa mali hizo wamemkabidhi Bi Katherine kiasi cha dola 55 milioni sawa na tsh 141 bilioni ikiwa ni sehemu ya mali za mwanaye.
Kwa mujibu wa TMZ imeeleza kuwa siku jana wasimamizi wa mali za MJ walifika ofisini kwao na kuwaonesha hati ya makabithiano ya mali hizo.
Ambapo Katherine Jackson amekabidhiwa kiasi hicho cha pesa ambacho kimekusanywa ndani ya miaka 15 tangu mwanaye MJ alipofariki Juni mwaka 2009.
Ikumbukwe kuwa siku ya Jana Machi 21, mtoto wa mwisho wa MJ, Bigi Jackson maarufu kama MJ Blanket (22) aliwasilisha ombi katika mahakama nchini humo kutomruhusu bibi yake kutumia pesa za MJ kwa ajili ya kukata rufaa kutokana na kutoona kama kesi hiyo itashinda.