pmbet

"Mama wa Taifa atasema Jambo hivi Karibuni" - Dkt Mpango

Sisti Herman

May 1, 2024
Share :

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango amesema ameagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwafikishia salamu wafanyakazi wote katika maadhimisho ya Mei Mosi kwamba kama hali ya kiuchumi ikiendelea kuwa kama ilivyo, siku chache zijazo atasema jambo kuhusu nyongeza ya mishahara.

 

“Mama wa Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameniagiza kuwa endapo hali hii itaendelea wafanyakazi wawe na matumani na atasema jambo hivi karibuni, pamoja na hilo serikali imeendelea kuboresha maslahi ya watumishi kwa namna mbalimbali ikiwemo kulipa nyongeza ya mwaka ya mshahara” amesema Makamu wa Rais Dkt. Phillip Isdory Mpango.

 

Dk. Mpango ameyasema hayo jijini Arusha kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).

 

Kwenye Picha ni machache kati ya mabango yenye jumbe mbalimbali za wafanyakazi ikiwemo bango kuhusu Kikokotoo cha mafao ya wastaafu chenye ujumbe wao kwa serikali.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet