pmbet

Mamelodi watwaa Ubingwa Sauzi wakiinyuka Kaizer Chiefs 5-1

Sisti Herman

May 3, 2024
Share :

Mara baada ya kuinyuka Kaizer Chiefs 5-1 kwenye mchezo wao wa raundi ya 24 wa ligi kuu nchini Afrika kusini, klabu ya Mamelodi Sundwons imetawazwa kuwa mabingwa kwa mara saba mfululizo wa ligi hiyo baada ya kufikisha alama 62 ambazo haziwezi kufikiwa na wapinzani wao Stellenbosch wenye alama 49 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Mamelodi ambao wametawazwa mabingwa wakiwa na mechi 6 mkononi mabao dhidi ya Kaizer yamefungwa na Matias Esquivel, Tashreeq Maetheews aliyefunga mawili, Lucas Ribeiro na Thembinkosi Lorch huku bao la pekee la Kaizer likifungwa na Mduduzi Shabalala.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet