Mamia wapoteza ajira baada ya Jeshi kufungia vituo vya Radio na TV
Eric Buyanza
May 30, 2024
Share :
Mamia ya watu wamepoteza ajira zao baada ya utawala wa kijeshi nchini Guinea kuvifungia vituo vinne vya Redio na viwili vya Televisheni.
Hayo yameelezwa na muungano wa vyombo vya habari ambao unajiandaa kuitisha mgomo wa nchi nzima.
Muungano huo umetishia kuanzisha mgomo wa nchi nzima usiokuwa na kikomo baada ya mamlaka nchini Guinea kufuta leseni za uendeshaji wa shughuli za vituo sita vya habari wakati nchi hiyo ikiwa inakabiliwa na mazingira mabaya ya kisiasa.
Mamlaka zimesema kufungiwa vituo hivyo vya habari kumetokana na vyombo hivyo kushindwa kutekeleza maagizo kuhusu maudhui wanayorusha hewani.