pmbet

Mamilioni ya watu hataraini kufa kisa misaada ya USAID

Sisti Herman

July 15, 2025
Share :



Nchi 132 ambazo zilikuwa zikinufaika moja kwa moja na ufadhili kutoka kwa Shirika la Misaada la Marekani (USAID), ziko hatarini kupoteza jumla ya watu 14 milioni kufikia mwaka 2030 baada ya kufungwa rasmi kwa shirika hilo la kutoa misaada.

Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la sayansi la Lancet unaeleza kwa kina jinsi hatua zilizopigwa katika miongo miwili iliyopita kupunguza vifo vya watoto na watu wazima,  zinavyoweza kuporomoka kufutia hatua hiyo.

“Makadirio yetu yanaonyesha kuwa, kama hatua za kupunguza ufadhili zilizotangazwa na kutekelezwa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025 hazitaondolewa, idadi kubwa ya vifo vinavyoweza kuepukika vinaweza kutokea kufikia mwaka 2030,” wamesema watafiti.

Tofauti na kazi za utafiti za awali ambazo zilijikita tu kwenye athari za moja kwa moja za kiafya, utafiti huu mpya umeangazia pia athari mbadala ambazo pia zinaweza kusababisha vifo na kupoteza njia za kujikimu, na kueleza kuwa pia zinaathiri afya ya watu.

Mipango isiyo ya afya iliyofadhiliwa ni pamoja na misaada ya kifedha, kupunguza umaskini, elimu, na miradi ya maji na usafi wa mazingira.

“Makadirio yetu mara nyingi huwa juu zaidi kwa sababu yanazingatia si tu athari za moja kwa moja za miradi ya afya ya USAID kama tafiti za awali, bali pia athari pana za misaada ya USAID. Athari hizi zinaweza kuwa zimechangia sana katika mafanikio ya shirika hili kupunguza vifo,” wameeleza.

Wanasayansi hao wamesema kati ya mwaka 2000 na 2023, vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano vilipungua kutoka 10.1 milioni hadi 4.8 milioni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet