pmbet

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari ya Mvua

Sisti Herman

April 22, 2024
Share :

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa na ngurumo kwa mikoa 26 ya Tanzania Bara na visiwa vya Unguja na Pemba kaunzia leo Aprili 22,2024.

Mikoa inayopata mvua leo kwa mujibu wa TMA ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro,Lindi, Mtwara, Kigoma , Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara ,Dodoma, Singida, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe pamoja na Unguja na Pemba.

“Angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya Mkoa wa Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba,” imeandikwa kwenye taarifa hiyo ya matarajio ya hali mbaya ya hewa ya siku tano kuanzia jana Aprili 21, 2024.

Kwa siku ya leo angalizo la uwepo wa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa kufikia mita mbili, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

Kiwango cha athari ambayo imeelezwa na TMA kutokana na mvua hizo ni wastani.

Aprili 23, TMA kupitia taarifa hiyo walitoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mkoa ya Dar es SSalaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet