Man City kushushwa daraja
Joyce Shedrack
January 22, 2024
Share :
Klabu ya Manchestet City huwenda ikaondolewa kushiriki Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa watakutwa na hatia ya mashitaka ya makosa 115 yanayowakabili ya kuvunja kanuni za Uendeshaji wa vilabu vya EPL.
Afisa mkuu wa zamani wa fedha wa Ligi Kuu ya Uingereza Stefan Borson alionya kwamba hii ni kwa kiwango tofauti kabisa na kile kilichotokea kwa Everton na Nottingham Forest.
"Klabu (Man City) inaweza kufungiwa kushiriki Ligi Kuu ya Uingereza kwa kipindi cha mwaka 1 hadi 10, ambao ndio muda ambao walidaiwa kuvunja sheria za FFP na hakuna anayeweza kupinga adhabu hiyo kisheria."
Hii itakuwa adhabu kubwa zaidi kuikumba Man City katika historia yao,
Mpaka sasa Man City ipo nafasi 2 katika msimamo wa ligi kuu ya uingereza wakiwa wamecheza michezo 20 na kukusanya alama 43 nyuma ya liverpool anayeongoza kwa alama 48 katika michezo 21 aliyocheza msimu huu .