Man City na Bouaddi wafikia makubaliano
Sisti Herman
August 10, 2026
Share :

Klabu ya Manchester City imeripotiwa kufikia makubaliano ya kibinafsi na kiungo wa kati Ayyoub Bouaddi kwaajili ya kujiunga nao kwenye dirisha hili la usajili.
Kwa mujibu wa ripoti ya Fabrizio Romano, Kiungo huyo wa Morocco mwenye umri wa miaka 18 ameridhia uhamisho huo na mkataba uko tayari baada ya mazungumzo na mawakala pamoja na familia yake.
Sasa Man City itasonga mbele kukamilisha dili hilo na klabu ya Lille hivi karibuni.
Bouaddi anapendelea kujiunga na kikosi cha City 𝐒𝐀𝐒𝐀 yaani msimu huu badala ya kusubiri hadi majira ya joto ya mwaka 2027 kama ilivyopangwa awali.





