Man City waanza mapemaaa mazungumzo ya mkataba na Ederson
Eric Buyanza
March 18, 2024
Share :
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil amejijengea sifa ya kuwa mmoja wa makipa bora zaidi duniani tangu ajiunge na Man City akitokea Benfica mwaka 2017.
Ederson amecheza zaidi ya mechi 325 katika kipindi chake akiwa na Citizens, akiisaidia klabu hiyo kushinda mataji matano ya Ligi Kuu, kombe la Ligi ya Mabingwa, Vikombe viwili vya FA, Vikombe vinne vya EFL, UEFA Super Cup na Kombe la Dunia la Klabu.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star, Man City wanajiandaa kufanya mazungumzo ya kwa ajili ya kumuongezea mkataba golikipa huyo ambaye hata hivyo bado ana mkataba unaoisha Juni 2026.
Hata hivyo, mabingwa hao wa Ulaya wanaamini ni jambo la maana kuanza mazungumzo juu ya mkataba mpya haraka iwezekanavyo.
Ederson anatajwa kulipwa kiasi cha pauni 120,000 kwa wiki, Man City wako tayari kuongeza kiasi hicho hadi pauni 200,000 huku wakimfunga mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kwenye mkataba wa muda mrefu.
Ederson, ambaye amecheza mechi 27 msimu huu, kwa sasa hayupo uwanjani baada ya kupata jeraha wakati Man City wakitoka sare ya 1-1 dhidi ya Liverpool wikiendi iliyopita.