pmbet

Man city wafanya mazungumzo na Enzo Maresca

Eric Buyanza

April 24, 2026
Share :

Manchester City wamefanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Chelsea, Enzo Maresca, kuona kama atakubali kurithi mikoba ya Pep Guardiola ambaye mustakabali wake ndani ya Etihad bado haueleweki.

 

Guardiola kwasasa yuko katika miezi ya mwisho ya mkataba wake na City, hivyo uongozi wa klabu hiyo umeanza harakati za kuandaa mrithi.

 

Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian, jina la Maresca linaonekana kuwa chaguo la kwanza miongoni mwa wengi wanaotajwa kwa ajili ya kazi hiyo.

 

Haya yanajiri huku kukiwa na uvumi kwamba Guardiola ataweza kuondoka msimu huu wa joto, hata hivyo City bado wana matumaini kuwa atamaliza kandarasi yake hadi 2027, lakini pia hawataki 'ku-risk'.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet