Man City wameanza mazungumzo ya kumsajili Rayan Ait-Nouri
Eric Buyanza
April 16, 2024
Share :
Manchester City wamefanya mazungumzo na Wolverhampton Wanderers kuhusu uwezekano wa kumnunua beki wa klabu hiyo Rayan Ait-Nouri.
Ait-Nouri mwenye umri wa miaka 22, amekuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu kama beki wa kushoto na tayari amevivutia vilabu vikubwa vya Premier League.
Arsenal na Liverpool pia wako kwenye mawindo na wanamfuatilia kwa karibu mlinzi huyo wa Algeria, ingawa harakati za Man City zinaweza kusaidiwa na uhusiano wao mzuri na Jorge Mendes (wakala wa Ait-Nouri).