Man City wamsajili mrithi wa Messi Argentina
Sisti Herman
January 26, 2024
Share :
Manchester City imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Claudio Echeverri kwa ada ya pauni milioni 12.5 kutoka klabu ya River Plate ya Argentina.
Kinda huyo mzaliwa wa 2006 anatajwa kuwa mmoja wa warithi wa Mchezaji bora wa nchi hiyo kwa sasa Lionel Messi siku za usoni kwani alikiwasha sana kwenye kombe la dunia la vijana chini ya umri wa miaka 17 huku akiwafunga mabao matatu kwenye mchezo wa robo fainali mahasimu wao wakubwa Brazil.
Echeverri (18) raia wa Argentina amesaini mkataba mpaka Juni 2028 lakini anasalia River Plate kwa mkopo mpaka Januari 2025 kabla ya kujiunga rasmi na Mabingwa hao watetezi wa EPL.