Man City wanasa saini ya beki Khusanov kutoka Lens
Sisti Herman
January 20, 2025
Share :
Klabu ya Manchester City imekamilisha rasmi taratibu za uhamisho wa beki wa kati wa kimataifa wa Uzbekistan, Abdukodir Khikmatovich Khusanov kutokea klabu ya Lens ya ligi kuu ya Ufaransa.
Man City imemnasa beki huyo shoka mwenye umri wa miaka 20 kwa ada ya uhamisho ya Paundi Milioni 33 (zaidi ya Tsh Bilioni 100).
Beki huyo amesaini mkataba wa miaka minne kuitumikia klabu hiyo.