Man City wanauza mitumba ya Guardiola kwa pesa ndefu
Sisti Herman
July 26, 2026
Share :

Baadhi ya vitu maalum vilivyoachwa na Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City vinauzwa kwa mnada wiki hii, huku mapato yote yakielekezwa kwa taasisi ya hisani ya 'City in the Community' shirika rasmi la klabu hiyo linalojihusisha na shughuli za kijamii.
Klabu imetengeneza ofisi ya mtandaoni ili kuruhusu watu wanaotaka kushiriki mnada "kuchunguza" eneo hilo, ambalo lina vitu binafsi kutoka ofisini kwake, mavazi aliyotumia wakati wa mechi na mazoezi, pamoja na vitu vya kumbukumbu.
Hii ni fursa adimu ya kumiliki kipande cha historia kutoka katika mojawapo ya vipindi vya mafanikio makubwa zaidi katika historia ya soka la Uingereza.





