Man City watwaa taji la EPL kwa mara ya 4 mfululizo
Sisti Herman
May 19, 2024
Share :
Mara baada ya kushinda 3-1 dhidi ya West Ham kwenye mchezo wao wa mwisho leo, klabu ya Manchester City imetwaa taji la ligi kuu nchini Uingereza kwa mara ya nne mfululizo na kuwa klabu ya kwanza kufanya hivyo katika historia.
Man City imetwaa taji hilo baada ya kufikisha alama 91 na kuwazidi washindani wao Arsenal ambao licha ya kushinda 2-1 dhidi ya Everton wameishia alama 89.
Huo unakuwa ubingwa wa 6 kati ya misimu 7 ya Guardiola kwenye ligi hiyo.