Man City yaangukia pua mataji matano waliyoshiriki msimu huu.
Joyce Shedrack
July 1, 2025
Share :
Klabu ya Manchester City ni rasmi wamemaliza msimu huu bila kutwaa taji lolote baada ya kutupwa nje kwenye mashindano ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu alfajiri ya leo na Al Hilal.
Man City imeondoshwa katika mashindano hayo kufuatia kipigo cha magoli 4-3 dhidi Al Hilal waliofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali na kuifanya klabu hiyo kukosa jumla ya makombe matano walioshiriki msimu huu ikiwemo ligi kuu ya Uingereza,Michuano ya Carabao,Kombe la FA,na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Al Hilal itakutana na Fluminense ya Brazil waliofanikiwa kuwaondosha Inter Milan kwa kuwatandika mabao 2-0.