Man City yathibitisha Rodri kufanyiwa upasuaji wa Mgongo.
Joyce Shedrack
July 25, 2026
Share :
Kiungo nyota wa Manchester City na timu ya taifa ya Hispania Rodri anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mgongo siku ya Jumatatu baada ya kusumbuliwa na tatizo la mgongo, klabu ya Manchester City imethibitisha.

Kocha mpya wa Manchester City, Enzo Maresca, amesema Rodri anahitaji muda wa kupumzika na kupona kikamilifu kabla ya kurejea uwanjani.
"Rodri atafanyiwa upasuaji wa tatizo wa mgongo anahitaji mapumziko muda wa kupona, kisha atarejea nasi. Kila kocha angependa kuwa na Rodri, ni mchezaji wa kiwango cha juu," amesema Maresca.
Licha ya kuandamwa na maumivu ya mgongo, Rodri aliendelea kuonyesha kiwango bora katika Kombe la Dunia, akiiwezesha Hispania kutwaa ubingwa na pia kutunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano (Player of the Tournament).
Nyota huyo siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa kuhitajika na Mabingwa mara nyingi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Real Madrid.





