Man U kwenye vita ya kugombea saini ya Kvaratskhelia
Eric Buyanza
January 10, 2025
Share :
Manchester United iko tayari kuchuana na Paris St-Germain pamoja na Liverpool ili kuinasa saini ya mshambuliajii wa Napoli, Khvitcha Kvaratskhelia.
Taarifa zinasema wakati Manchester United ikiweka nia ya kumtaka Kvaratskhelia, klabu za PSG na Liverpool nao wamekuwa wakimfuatilia kwa ukaribu winga huyo kutoka Georgia. Kvaratskhelia mwenye umri wa miaka 23 amekuwa na kiwango bora na klabu yake na staili ya uchezaji wake umezivutia klabu nyingi barani ulaya. Kwa mujibu wa Transfermarkt, thamani ya winga huyo inafikia Euro milioni 85.