Man U yachomoa mazungumzo mapya dili la Rashford
Eric Buyanza
February 18, 2026
Share :
Manchester United imethibitisha kuwa haitafanya mazungumzo mapya kuhusu bei ya uhamisho wa Marcus Rashford kwenda Barcelona.
Rashford, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo wa msimu mzima huko Barcelona, anaweza kununuliwa kwa pauni milioni 26 mwishoni mwa msimu huu.
Barcelona ilikuwa inataka kupunguza bei hiyo, lakini Manchester United imesema haitafanya mazungumzo yoyote mapya na inataka kulipwa kiasi chote kilichokubaliwa.
Rashford amefanya vizuri huko Barcelona, akifunga magoli 10 na kutoa asisti 13 katika michezo 34.






