Man U yamtaka Myles Lewis-Skelly, Arteta asema: "Haendi popote!"
Eric Buyanza
August 25, 2026
Share :

Manchester United wanajaribu kuishawishi Arsenal ili waweze kumuachia kinda Myles Lewis-Skelly.
Skelly mwenye umri wa miaka 19 ana uwezo wa kucheza nafasi mbili kuu uwanjani, ambazo ni Beki wa Kushoto (Left-back) na Kiungo wa Kati (Central/Defensive Midfielder).
Hata hivyo Arsenal wameweka ngumu na wanaripotiwa kuhitaji kiasi cha pauni milioni 50 (takribani Bilioni 180 za Kitanzania) ili kumuachia, lakini United wanaona kiasi hicho ni kikubwa mno kwa kijana huyo.
Uwezo wake wa kumudu nafasi mbili kwa ufasaha ndio unaomfanya athaminiwe sana na Arsenal, na pia ndio sababu inayomfanya kocha wa Manchester United, Michael Carrick, kumfukuzia ili akasaidie matatizo ya beki wa kushoto na kuongeza nguvu kwenye kiungo cha United.
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amesisitiza hadharani kuwa ana uhakika wa 100% kwamba Lewis-Skelly atabaki klabuni hapo.





