Man United kumuachia Varane aondoke
Eric Buyanza
April 27, 2024
Share :
Manchester United wako tayari kumuachia Raphael Varane kuondoka klabuni hapo kama mchezaji huru.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 31 atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu na Manchester United hawana nia ya kumuongezea mkataba.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa analipwa mshahara mkubwa na 'Mashetani wekundu' wanataka kumuondoa kwenye daftari lao.