Man United na Liverpool kwenye mbio za kumgombea Odilon Kossounou
Eric Buyanza
May 20, 2024
Share :
Manchester United wanataka kumsajili beki wa Bayer Leverkusen, Odilon Kossounou mwishoni mwa msimu huu.
Taarifa zinasema Man U wanaongoza mbio za kuwania saini ya mchezaji huyo, lakini wanakabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao Liverpool.
Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 23 amekuwa tegemeo kwenye klabu yake na aina ya uchezaji wake umezivutia klabu nyingi kubwa.